9 Umeweka mpaka yasiupite,Wala yasirudi kuifunikiza nchi.
10 Hupeleka chemchemi katika mabonde;Zapita kati ya milima;
11 Zamnywesha kila mnyama wa kondeni;Punda mwitu huzima kiu yao.
12 Kandokando hukaa ndege wa angani;Kati ya matawi hutoa sauti zao.
13 Huinywesha milima toka orofa zake;Nchi imeshiba mazao ya kazi zako.
14 Huyameesha majani kwa makundi,Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu;Ili atoe chakula katika nchi,
15 Na divai imfurahishe mtu moyo wake.Aung’aze uso wake kwa mafuta,Na mkate umburudishe mtu moyo wake.