1 Haleluya.Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake,Wajulisheni watu matendo yake.
2 Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi,Zitafakarini ajabu zake zote.
3 Jisifuni kwa jina lake takatifu,Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
4 Mtakeni BWANA na nguvu zake,Utafuteni uso wake sikuzote.
5 Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya,Miujiza yake na hukumu za kinywa chake.