10 Alilomthibitishia Yakobo liwe amri,Na Israeli liwe agano la milele.
11 Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani,Iwe urithi wenu mliopimiwa.
12 Walipokuwa watu wawezao kuhesabiwa,Naam, watu wachache na wageni ndani yake,
13 Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa,Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine.
14 Hakumwacha mtu awaonee,Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao.
15 Akisema, Msiwaguse masihi wangu,Wala msiwadhuru nabii zangu.
16 Akaiita njaa iijilie nchi,Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.