13 Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa,Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine.
14 Hakumwacha mtu awaonee,Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao.
15 Akisema, Msiwaguse masihi wangu,Wala msiwadhuru nabii zangu.
16 Akaiita njaa iijilie nchi,Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.
17 Alimpeleka mtu mbele yao,Yusufu aliuzwa utumwani.
18 Walimwumiza miguu yake kwa pingu,Akatiwa katika minyororo ya chuma.
19 Hata wakati wa kuwadia neno lake,Ahadi ya BWANA ilimjaribu.