16 Akaiita njaa iijilie nchi,Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.
17 Alimpeleka mtu mbele yao,Yusufu aliuzwa utumwani.
18 Walimwumiza miguu yake kwa pingu,Akatiwa katika minyororo ya chuma.
19 Hata wakati wa kuwadia neno lake,Ahadi ya BWANA ilimjaribu.
20 Mfalme alituma watu akamfungua,Mkuu wa watu akamwachia.
21 Akamweka kuwa bwana wa nyumba yake,Na mwenye amri juu ya mali zake zote.
22 Awafunge masheki wake kama apendavyo,Na kuwafundisha wazee wake hekima.