3 Jisifuni kwa jina lake takatifu,Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
4 Mtakeni BWANA na nguvu zake,Utafuteni uso wake sikuzote.
5 Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya,Miujiza yake na hukumu za kinywa chake.
6 Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake;Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
7 Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu;Duniani mwote mna hukumu zake.
8 Analikumbuka agano lake milele;Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
9 Agano alilofanya na Ibrahimu,Na uapo wake kwa Isaka.