34 Alisema, kukaja nzige,Na tunutu wasiohesabika;
35 Wakaila miche yote ya nchi yao,Wakayala matunda ya ardhi yao.
36 Akawapiga wazaliwa wa kwanza katika nchi,Malimbuko ya nguvu zao.
37 Akawatoa hali wana fedha na dhahabu,Katika kabila zao asiwepo mwenye kukwaa.
38 Misri ilifurahi walipoondoka,Maana kwa ajili yao hofu imewaangukia.
39 Alitandaza wingu liwe funiko,Na moto utoe nuru usiku.
40 Walipotaka akaleta kware,Akawashibisha chakula cha mbinguni.