36 Akawapiga wazaliwa wa kwanza katika nchi,Malimbuko ya nguvu zao.
37 Akawatoa hali wana fedha na dhahabu,Katika kabila zao asiwepo mwenye kukwaa.
38 Misri ilifurahi walipoondoka,Maana kwa ajili yao hofu imewaangukia.
39 Alitandaza wingu liwe funiko,Na moto utoe nuru usiku.
40 Walipotaka akaleta kware,Akawashibisha chakula cha mbinguni.
41 Akaufunua mwamba, kukabubujika maji,Yakapita pakavuni kama mto.
42 Maana alilikumbuka neno lake takatifu,Na Ibrahimu, mtumishi wake.