37 Akawatoa hali wana fedha na dhahabu,Katika kabila zao asiwepo mwenye kukwaa.
38 Misri ilifurahi walipoondoka,Maana kwa ajili yao hofu imewaangukia.
39 Alitandaza wingu liwe funiko,Na moto utoe nuru usiku.
40 Walipotaka akaleta kware,Akawashibisha chakula cha mbinguni.
41 Akaufunua mwamba, kukabubujika maji,Yakapita pakavuni kama mto.
42 Maana alilikumbuka neno lake takatifu,Na Ibrahimu, mtumishi wake.
43 Akawatoa watu wake kwa shangwe,Na wateule wake kwa nyimbo za furaha.