1 Haleluya.Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA,Kuzihubiri sifa zake zote?
3 Heri washikao hukumu,Na kutenda haki sikuzote.
4 Ee BWANA, unikumbuke mimi,Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.Unijilie kwa wokovu wako,
5 Ili niuone wema wa wateule wako.Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako,Na kujisifu pamoja na watu wako.
6 Tumetenda dhambi pamoja na baba zetu,Tumetenda maovu, tumefanya ubaya.