14 Bali walitamani sana jangwani,Wakamjaribu Mungu nyikani.
15 Akawapa walichomtaka,Akawakondesha roho zao.
16 Wakamhusudu Musa matuoni,Na Haruni, mtakatifu wa BWANA.
17 Nchi ikapasuka ikammeza Dathani,Ikaufunika mkutano wa Abiramu.
18 Moto ukawaka katika mkutano wao,Miali yake ikawateketeza wabaya.
19 Walifanya ndama huko Horebu,Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.
20 Wakaubadili utukufu waoKuwa mfano wa ng’ombe mla majani.