18 Moto ukawaka katika mkutano wao,Miali yake ikawateketeza wabaya.
19 Walifanya ndama huko Horebu,Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.
20 Wakaubadili utukufu waoKuwa mfano wa ng’ombe mla majani.
21 Wakamsahau Mungu, mwokozi wao,Aliyetenda makuu katika Misri.
22 Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu,Mambo ya kutisha penye bahari ya Shamu.
23 Akasema ya kuwa atawaangamizaKama Musa, mteule wake, asingalisimama,Mbele zake kama mahali palipobomoka,Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.
24 Wakaidharau nchi ile ya kupendeza,Wala hawakuliamini neno lake.