25 Bali wakanung’unika hemani mwao,Wala hawakuisikiliza sauti ya BWANA.
26 Ndipo alipowainulia mkono wake,Ya kuwa atawaangamiza jangwani,
27 Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa,Na kuwatapanya katika nchi mbali.
28 Wakajiambatiza na Baal-Peori,Wakazila dhabihu za wafu.
29 Wakamkasirisha kwa matendo yao;Tauni ikawashambulia.
30 Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu;Tauni ikazuiliwa.
31 Akahesabiwa kuwa ana hakiKizazi baada ya kizazi hata milele.