26 Ndipo alipowainulia mkono wake,Ya kuwa atawaangamiza jangwani,
27 Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa,Na kuwatapanya katika nchi mbali.
28 Wakajiambatiza na Baal-Peori,Wakazila dhabihu za wafu.
29 Wakamkasirisha kwa matendo yao;Tauni ikawashambulia.
30 Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu;Tauni ikazuiliwa.
31 Akahesabiwa kuwa ana hakiKizazi baada ya kizazi hata milele.
32 Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba,Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,