3 Heri washikao hukumu,Na kutenda haki sikuzote.
4 Ee BWANA, unikumbuke mimi,Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.Unijilie kwa wokovu wako,
5 Ili niuone wema wa wateule wako.Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako,Na kujisifu pamoja na watu wako.
6 Tumetenda dhambi pamoja na baba zetu,Tumetenda maovu, tumefanya ubaya.
7 Baba zetu katika MisriHawakufikiri matendo yako ya ajabu;Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako;Wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu.
8 Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake,Ayadhihirishe matendo yake makuu.
9 Akaikemea bahari ya Shamu ikakauka,Akawaongoza vilindini kana kwamba ni uwanda.