31 Akahesabiwa kuwa ana hakiKizazi baada ya kizazi hata milele.
32 Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba,Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,
33 Kwa sababu waliiasi roho yake,Akasema yasiyofaa kwa midomo yake.
34 Hawakuwaharibu watu wa nchiKama BWANA alivyowaambia;
35 Bali walijichanganya na mataifa,Wakajifunza matendo yao.
36 Wakazitumikia sanamu zao,Nazo zikawa mtego kwao.
37 Naam, walitoa wana wao na binti zaoKuwa dhabihu kwa mashetani.