9 Akaikemea bahari ya Shamu ikakauka,Akawaongoza vilindini kana kwamba ni uwanda.
10 Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia,Na kuwakomboa na mkono wa adui zao.
11 Maji yakawafunika watesi wao,Hakusalia hata mmoja wao.
12 Ndipo walipoyaamini maneno yake,Waliziimba sifa zake.
13 Wakayasahau matendo yake kwa haraka,Hawakulingojea shauri lake.
14 Bali walitamani sana jangwani,Wakamjaribu Mungu nyikani.
15 Akawapa walichomtaka,Akawakondesha roho zao.