1 Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,Nitaimba, nitaimba zaburi,Naam, kwa utukufu wangu.
2 Amka, kinanda na kinubi,Nitaamka alfajiri.
3 Ee BWANA, nitakushukuru kati ya watu,Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.
4 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,Na uaminifu wako hata mawinguni.
5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6 Ili wapenzi wako waopolewe,Uokoe kwa mkono wako wa kuume, uniitikie.