2 Amka, kinanda na kinubi,Nitaamka alfajiri.
3 Ee BWANA, nitakushukuru kati ya watu,Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.
4 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,Na uaminifu wako hata mawinguni.
5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6 Ili wapenzi wako waopolewe,Uokoe kwa mkono wako wa kuume, uniitikie.
7 Mungu amenena kwa utakatifu wake,Nami nitashangilia.Nitaigawanya Shekemu,Nitalipima bonde la Sukothi.
8 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu.Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,