1 Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze,
2 Kwa maana wamenifumbulia kinywa;Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila,Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.
3 Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka,Wamepigana nami bure.
4 Badala ya upendo wangu wao hunishitaki,Ijapokuwa naliwaombea.
5 Wamenichukuza mabaya badala ya mema,Na chuki badala ya upendo wangu.
6 Uweke mtu mkorofi juu yake,Mshitaki asimame mkono wake wa kuume.
7 Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki,Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.