20 Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa BWANA,Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.
21 Na Wewe, MUNGU, Bwana, unitendee kwa ajili ya jina lako,Kwa kuwa fadhili zako ni njema uniokoe.
22 Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji,Na moyo wangu umejeruhi ndani yangu.
23 Ninapita kama kivuli kianzacho kutoweka,Ninapeperushwa kama nzige.
24 Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga,Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.
25 Nami nalikuwa laumu kwao,Wanionapo hutikisa vichwa vyao.
26 Ee BWANA, Mungu wangu, unisaidie,Uniokoe sawasawa na fadhili zako.