22 Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji,Na moyo wangu umejeruhi ndani yangu.
23 Ninapita kama kivuli kianzacho kutoweka,Ninapeperushwa kama nzige.
24 Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga,Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.
25 Nami nalikuwa laumu kwao,Wanionapo hutikisa vichwa vyao.
26 Ee BWANA, Mungu wangu, unisaidie,Uniokoe sawasawa na fadhili zako.
27 Nao wakajue ya kuwa ndio mkono wako;Wewe, BWANA, umeyafanya hayo.
28 Wao walaani, bali Wewe utabariki,Wameondoka wao wakaaibishwa,Bali mtumishi wako atafurahi.