3 Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka,Wamepigana nami bure.
4 Badala ya upendo wangu wao hunishitaki,Ijapokuwa naliwaombea.
5 Wamenichukuza mabaya badala ya mema,Na chuki badala ya upendo wangu.
6 Uweke mtu mkorofi juu yake,Mshitaki asimame mkono wake wa kuume.
7 Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki,Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.
8 Siku zake na ziwe chache,Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.
9 Wanawe na wawe yatima,Na mkewe na awe mjane.