1 BWANA ndiye niliyemkimbilia.Mbona mnaiambia nafsi yangu,Kimbia kama ndege mlimani kwenu?
2 Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta,Wanaitia mishale yao katika upote,Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.
3 Kama misingi ikiharibika,Mwenye haki atafanya nini?
4 BWANA yu katika hekalu lake takatifu.BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni,Macho yake yanaangalia;Kope zake zinawajaribu wanadamu.