3 Kama misingi ikiharibika,Mwenye haki atafanya nini?
4 BWANA yu katika hekalu lake takatifu.BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni,Macho yake yanaangalia;Kope zake zinawajaribu wanadamu.
5 BWANA humjaribu mwenye haki;Bali nafsi yake humchukia asiye haki,Na mwenye kupenda udhalimu.
6 Awanyeshee wasio haki mitego,Moto na kiberiti na upepo wa hari,Na viwe fungu la kikombe chao.