1 Haleluya.Enyi watumishi wa BWANA, sifuni,Lisifuni jina la BWANA.
2 Jina la BWANA lihimidiweTangu leo na hata milele.
3 Toka maawio ya jua hata machweo yakeJina la BWANA husifiwa.
4 BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,Na utukufu wake ni juu ya mbingu.