3 Bahari iliona ikakimbia,Yordani ilirudishwa nyuma.
4 Milima iliruka kama kondoo waume,Vilima kama wana-kondoo.
5 Ee bahari, una nini, ukimbie?Yordani, urudi nyuma?
6 Enyi milima, mruke kama kondoo waume?Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7 Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana,Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.