1 Haleluya.Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikilizaSauti yangu na dua zangu.
2 Kwa maana amenitegea sikio lake,Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.
3 Kamba za mauti zilinizunguka,Shida za kuzimu zilinipata.Naliona taabu na huzuni;
4 Nikaliitia jina la BWANA.Ee BWANA, nakuomba sana,Uniokoe nafsi yangu.
5 BWANA ni mwenye neema na haki,Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.
6 BWANA huwalinda wasio na hila;Nalidhilika, akaniokoa.
7 Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako,Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu.