5 BWANA ni mwenye neema na haki,Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.
6 BWANA huwalinda wasio na hila;Nalidhilika, akaniokoa.
7 Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako,Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu.
8 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti,Macho yangu na machozi,Na miguu yangu na kuanguka.
9 Nitaenenda mbele za BWANAKatika nchi za walio hai.
10 Naliamini, kwa maana nitasema,Mimi naliteswa sana.
11 Mimi nalisema kwa haraka yangu,Wanadamu wote ni waongo.