9 Nitaenenda mbele za BWANAKatika nchi za walio hai.
10 Naliamini, kwa maana nitasema,Mimi naliteswa sana.
11 Mimi nalisema kwa haraka yangu,Wanadamu wote ni waongo.
12 Nimrudishie BWANA niniKwa ukarimu wake wote alionitendea?
13 Nitakipokea kikombe cha wokovu;Na kulitangaza jina la BWANA;
14 Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,Naam, mbele ya watu wake wote.
15 Ina thamani machoni pa BWANAMauti ya wacha Mungu wake.