1 Haleluya.Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 Israeli na aseme sasa,Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
3 Mlango wa Haruni na waseme sasa,Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
4 Wamchao BWANA na waseme sasa,Ya kwamba fadhili zake ni za milele.