12 Walinizunguka kama nyuki,Walizimika kama moto wa miibani;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
13 Ulinisukuma sana ili nianguke;Lakini BWANA akanisaidia.
14 BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu,Naye amekuwa wokovu wangu.
15 Sauti ya furaha na wokovuImo hemani mwao wenye haki;Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.
16 Mkono wa kuume wa BWANA umetukuzwa;Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.
17 Sitakufa bali nitaishi,Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.
18 BWANA ameniadhibu sana,Lakini hakuniacha nife.