17 Sitakufa bali nitaishi,Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.
18 BWANA ameniadhibu sana,Lakini hakuniacha nife.
19 Nifungulieni malango ya haki,Nitaingia na kumshukuru BWANA.
20 Lango hili ni la BWANA,Wenye haki ndio watakaoliingia.
21 Nitakushukuru kwa maana umenijibu,Nawe umekuwa wokovu wangu.
22 Jiwe walilolikataa waashiLimekuwa jiwe kuu la pembeni.
23 Neno hili limetoka kwa BWANA,Nalo ni ajabu machoni petu.