21 Nitakushukuru kwa maana umenijibu,Nawe umekuwa wokovu wangu.
22 Jiwe walilolikataa waashiLimekuwa jiwe kuu la pembeni.
23 Neno hili limetoka kwa BWANA,Nalo ni ajabu machoni petu.
24 Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA,Tutashangilia na kuifurahia.
25 Ee BWANA, utuokoe, twakusihi;Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi.
26 Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA;Tumewabarikia toka nyumbani mwa BWANA.
27 BWANA ndiye aliye Mungu,Naye ndiye aliyetupa nuru.Ifungeni dhabihu kwa kambaPembeni mwa madhabahu.