25 Ee BWANA, utuokoe, twakusihi;Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi.
26 Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA;Tumewabarikia toka nyumbani mwa BWANA.
27 BWANA ndiye aliye Mungu,Naye ndiye aliyetupa nuru.Ifungeni dhabihu kwa kambaPembeni mwa madhabahu.
28 Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru,Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza.