4 Wamchao BWANA na waseme sasa,Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
5 Katika shida yangu nalimwita BWANA;BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.
6 BWANA yuko upande wangu, sitaogopa;Mwanadamu atanitenda nini?
7 BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu,Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
8 Ni heri kumkimbilia BWANAKuliko kuwatumainia wanadamu.
9 Ni heri kumkimbilia BWANA.Kuliko kuwatumainia wakuu.
10 Mataifa yote walinizunguka;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.