6 BWANA yuko upande wangu, sitaogopa;Mwanadamu atanitenda nini?
7 BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu,Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
8 Ni heri kumkimbilia BWANAKuliko kuwatumainia wanadamu.
9 Ni heri kumkimbilia BWANA.Kuliko kuwatumainia wakuu.
10 Mataifa yote walinizunguka;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
11 Walinizunguka, naam, walinizunguka;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
12 Walinizunguka kama nyuki,Walizimika kama moto wa miibani;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.