1 Heri walio kamili njia zao,Waendao katika sheria ya BWANA.
2 Heri wazitiio shuhuda zake,Wamtafutao kwa moyo wote.
3 Naam, hawakutenda ubatili,Wamekwenda katika njia zake.
4 Wewe umetuamuru mausia yako,Ili sisi tuyatii sana.
5 Ningependa njia zangu ziwe thabiti,Nizitii amri zako.
6 Ndipo mimi sitaaibika,Nikiyaangalia maagizo yako yote.