101 Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya,Ili nilitii neno lako.
102 Sikujiepusha na hukumu zako,Maana Wewe mwenyewe umenifundisha.
103 Mausia yako ni matamu sana kwangu,Kupita asali kinywani mwangu.
104 Kwa mausia yako najipatia ufahamu,Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
105 Neno lako ni taa ya miguu yangu,Na mwanga wa njia yangu.
106 Nimeapa nami nitaifikiliza,Kuzishika hukumu za haki yako.
107 Nimeteswa mno;Ee BWANA, unihuishe sawasawa na neno lako.