105 Neno lako ni taa ya miguu yangu,Na mwanga wa njia yangu.
106 Nimeapa nami nitaifikiliza,Kuzishika hukumu za haki yako.
107 Nimeteswa mno;Ee BWANA, unihuishe sawasawa na neno lako.
108 Ee BWANA, uziridhie sadaka za kinywa changu,Na kunifundisha hukumu zako.
109 Nafsi yangu imo mkononi mwangu daima,Lakini sheria yako sikuisahau.
110 Watendao uovu wamenitegea mtego,Lakini sikuikosa njia ya mausia yako.
111 Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele,Maana ndizo changamko la moyo wangu.