109 Nafsi yangu imo mkononi mwangu daima,Lakini sheria yako sikuisahau.
110 Watendao uovu wamenitegea mtego,Lakini sikuikosa njia ya mausia yako.
111 Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele,Maana ndizo changamko la moyo wangu.
112 Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako,Daima, naam, hata milele.
113 Watu wa kusita-sita nawachukia,Lakini sheria yako naipenda.
114 Ndiwe sitara yangu na ngao yangu,Neno lako nimelingojea.
115 Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu,Niyashike maagizo ya Mungu wangu.