111 Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele,Maana ndizo changamko la moyo wangu.
112 Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako,Daima, naam, hata milele.
113 Watu wa kusita-sita nawachukia,Lakini sheria yako naipenda.
114 Ndiwe sitara yangu na ngao yangu,Neno lako nimelingojea.
115 Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu,Niyashike maagizo ya Mungu wangu.
116 Unitegemeze sawasawa na ahadi yako, nikaishi,Wala usiniache niyaaibikie matumaini yangu.
117 Unisaidie nami nitakuwa salama,Nami nitaziangalia amri zako daima.