117 Unisaidie nami nitakuwa salama,Nami nitaziangalia amri zako daima.
118 Umewakataa wote wazikosao amri zako,Kwa maana hila zao ni uongo.
119 Wabaya wa nchi pia umewaondoa kama takataka,Ndiyo maana nimezipenda shuhuda zako.
120 Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe,Nami ninaziogopa hukumu zako.
121 Nimefanya hukumu na haki,Usiniache mikononi mwao wanaonionea.
122 Uwe mdhamini wa mtumishi wako, apate mema,Wenye kiburi wasinionee.
123 Macho yangu yamefifia kwa kuutamani wokovu wako,Na ahadi ya haki yako.