122 Uwe mdhamini wa mtumishi wako, apate mema,Wenye kiburi wasinionee.
123 Macho yangu yamefifia kwa kuutamani wokovu wako,Na ahadi ya haki yako.
124 Kama zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako,Na amri zako unifundishe.
125 Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe,Nipate kuzijua shuhuda zako.
126 Wakati umewadia BWANA atende kazi;Kwa kuwa wameitangua sheria yako.
127 Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako,Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi.
128 Maana nayaona mausia yako yote kuwa ya adili,Kila njia ya uongo naichukia.