128 Maana nayaona mausia yako yote kuwa ya adili,Kila njia ya uongo naichukia.
129 Shuhuda zako ni za ajabu,Ndiyo maana roho yangu imezishika.
130 Kufafanusha maneno yako kwatia nuru,Na kumfahamisha mjinga.
131 Nalifunua kinywa changu nikatweta,Maana naliyatamani maagizo yako.
132 Unigeukie, unirehemu mimi,Kama iwahusuvyo walipendao jina lako.
133 Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako,Uovu usije ukanimiliki.
134 Unikomboe na dhuluma ya mwanadamu,Nipate kuyashika mausia yako.