131 Nalifunua kinywa changu nikatweta,Maana naliyatamani maagizo yako.
132 Unigeukie, unirehemu mimi,Kama iwahusuvyo walipendao jina lako.
133 Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako,Uovu usije ukanimiliki.
134 Unikomboe na dhuluma ya mwanadamu,Nipate kuyashika mausia yako.
135 Umwangazie mtumishi wako uso wako,Na kunifundisha amri zako.
136 Macho yangu yachuruzika mito ya maji,Kwa sababu hawaitii sheria yako.
137 Ee BWANA, Wewe ndiwe mwenye haki,Na hukumu zako ni za adili.