134 Unikomboe na dhuluma ya mwanadamu,Nipate kuyashika mausia yako.
135 Umwangazie mtumishi wako uso wako,Na kunifundisha amri zako.
136 Macho yangu yachuruzika mito ya maji,Kwa sababu hawaitii sheria yako.
137 Ee BWANA, Wewe ndiwe mwenye haki,Na hukumu zako ni za adili.
138 Umeziagiza shuhuda zako kwa haki,Na kwa uaminifu mwingi.
139 Juhudi yangu imeniangamiza,Maana watesi wangu wameyasahau maneno yako.
140 Neno lako limesafika sana,Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.