14 Nimeifurahia njia ya shuhuda zakoKana kwamba ni mali mengi.
15 Nitayatafakari mausia yako,Nami nitaziangalia njia zako.
16 Nitajifurahisha sana kwa amri zako,Sitalisahau neno lako.
17 Umtendee mtumishi wako ukarimu,Nipate kuishi, nami nitalitii neno lako.
18 Unifumbue macho yangu niyatazameMaajabu yatokayo katika sheria yako.
19 Mimi ni mgeni katika nchi,Usinifiche maagizo yako.
20 Roho yangu imepondeka kwa kutamaniHukumu zako kila wakati.