140 Neno lako limesafika sana,Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.
141 Mimi ni mdogo, nadharauliwa,Lakini siyasahau mausia yako.
142 Haki yako ni haki ya milele,Na sheria yako ni kweli.
143 Taabu na dhiki zimenipata,Maagizo yako ni furaha yangu.
144 Haki ya shuhuda zako ni ya milele,Unifahamishe, nami nitaishi.
145 Nimeita kwa moyo wangu wote; Ee BWANA, uitike;Nitazishika amri zako.
146 Nimekuita Wewe, uniokoe,Nami nitazishika shuhuda zako.