142 Haki yako ni haki ya milele,Na sheria yako ni kweli.
143 Taabu na dhiki zimenipata,Maagizo yako ni furaha yangu.
144 Haki ya shuhuda zako ni ya milele,Unifahamishe, nami nitaishi.
145 Nimeita kwa moyo wangu wote; Ee BWANA, uitike;Nitazishika amri zako.
146 Nimekuita Wewe, uniokoe,Nami nitazishika shuhuda zako.
147 Kutangulia mapambazuko naliomba msaada,Naliyangojea maneno yako kwa tumaini.
148 Macho yangu yalitangulia makesha ya usiku,Ili kuitafakari ahadi yako.